Habari

Namna ya kuongoza na kusimamia watu usiowapenda

Wakati unafanya kazi na watu wengine ni kazi sana, lakini lazima ukumbuke namna ya kuhusiana nao. Wengine wanaweza kukasilishwa sana na makala hii kwakuwa unatakiwa kuwapenda watu unaowaongoza na kama unawapenda wengine zaidi inakuwa vizuri sana.

annoying-coworkers

Ukweli wa mambo ni kwamba kuna wakati utajikuta kuna watu umewachukia kazini na wako chini yako. Sizungumzii mtu ambaye anakusema vibaya au amekufanyia mambo baya ila ninamna tu jinsi alivyo anakuchukiza. Wewe kama kiongozi unafanyeje? Kuna baadhi ya vitu unatakiwa kuviangalia na kuvifanyia marekebisho kidogo;

1. Kwanza, tafuta tatizo lako ni nini?

Kama utendaji wao wa kazi unaridhisha na hilo ndio mambo lako la msingi hasa wewe kama kiongozi, hivyo una kazi ya ziada kuhakikisha unatafuta ni kitu gani hasa kinachokuudhi ndani ya hao watu unaowaongoza. Kama ni hulka binafsi na mitizamo yao hasi, kuna vitu huwezi kuvibadilisha ndani ya mtu kama yeye mwenyewe hajaamua kubadilika. kwahiyo mtu anayetakiwa kubadilika ni wewe mwenyewe na kuhakikisha unabadilika namna ambavyo unahusiana nao. Bila wewe kubadilika haitachukua muda mrefu wao kujua kwamba unawachukia na wafanyakazi wote katika kitu hicho watajua na kuathiri kitu kizima.

2. Haihitaji  wewe kuwa rafiki wa kila mfanyakazi wako.

Kuna utofauti mkubwa kati ya maisha ya kazini na maisha ya kawaida ya nyumbani katika ulimwengu wa biashara. Hakikisha unajenga uhusuano wenye afya na wafanyakazi wako na kuweka mipaka ya msingi kati yako na wao.

3. Wathamini kitaaluma zaidi

Unapokuwa mwanataaluma unataka watu wakuchukulie kwa staili fulani basi hivyo hivyo na wewe wachukulie hivyo. Unapokuwa nao onyesha kuwathamini kimazingira na kazi wanazofanya, hata kwenye maongezi ya kawaida usiingilile sana maisha yao nje ya kazi. Kwa lugha nyingine uwe mwangalifu unapozungumza nao au unapokuwa kwenye mazungumzo ambayo yanahusisha maisha nje ya kazi.

5. Usilete utani wa ndani

Kama una watu ambao wanakuudhi namna wanavyoongea au jinsi walivyo hapo kazi usimshirikishe mfanyakazi mwingine habari hiyo au namna unavyomchukulia mfanyakazi mwingine. Hii haifurahishi unapofanya hivyo unapoteza umaarufu wako hapo kazini kama kiongozi. Kwa ufupi tanya mambo na maamuzi ukizingatia usawa na heshima kwa wote. Vile vile uwe makini na maneno au sentensi unazotumia kwa jambo lolote au kitu chochote ambacho kinaweza kuibua sinto fahamu katika kazi.

6. Unatakiwa kujali umuhimu wao kwenye idara yenu

Mwisho wa siku, mfanyakazi huyo ana tija kwenye idara na mchango wake ni mkubwa na mzuri hivyo angalia thamani take na usimamie hapo. Hata kama kuna jambo limetokea ndani ya idara ambalo si zuri, litatue kwa kuangalia chanzo na msingi wake bila kuhusisha mambo yako binafsi dhidi ya wafanyakazi wako ukashindwa kushunghulikia mambo ya msingi.

Jambo la msingi ni kuzingatia kazi, usiruhusu kuendeshwa na hisia binafsi kwenye idara yako bali kusimamia malengo ya taasisi au jukumu lenu kama idara. Wewe kama kiongozi unahitajika kuwasimamia bila kuonyesha ubaguzi au chuki binafsi na watakuamini na kukuheshimu. Mambo mengine shughulikia madhaifu yako binafsi usiruhusu kuyaingiza kwa watu unaowaongoza.

Wanakuamini na kuamini uongozi wako, usifanye makosa yatakayosababisha wao kukuchukia au kuwa na mashaka na uongozi wako.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents