Habari

Namna ya kuongeza ufanisi katika kuwasiliana na watu

Mawasiliano huchukua zaidi ya asilimia  sabini (70%) katika maeneo ya kazi, hivyo unahitaji kuongeza uelewa wako na namna unavyowasiliana na kuchukua taarifa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Watu wengi wamekuwa wakikosana na wafanyakazi wenzao kila mara kwa sabu ya namna tuambavyo hawajui umuhimu wa kuwasiliana au hawakufundishwa hivyo hawajui mambo ya msingi katika kuwasiliana.

550791_483637455003610_580511176_n

Hahuhitaji shahada ya udhamili kujua namna ya kuwasiliana na wafanyakazi wenzako, unahitaji uelewa mpana katika kuwasiliana. ili kuongeza upana wa mawazo na maamuzi katika kuwasiliana, jaribu kufuatilia vipengele vifuatavyo;

1. Ongea kidogo na usikilize sana na kwa umakini mkubwa

Mara nyingi tunapenda kusikika kuliko kusikiliza, hivyo kupoteza agenda ya mazungumzo mengi kwa sababu tulikuwa hatusikilizi wengine. Tumekuwa tukiangalia agenda zetu kuliko kuangalia mwenzako anajaribu kuongea nini na umsikilize kwa umakini.

2. Usipambane na mleta habari au mjumbe wa hiyo habari

Tunahitaji kuelewa, uwezo wetu mwingi una mtizamo fulani wa kuchukulia mambo na kumtazama anayeongea au aliyeleta ujumbe na kutengeneza hukumu kwa anayeongea bila kuangalia ujumbe anaokupa kwa undani zaidi. Hivyo angalia ujumbe zaidi kuliko kuangalia kwanini ametumwa mjumbe huyu.

3. Epuka kusoma fikra za watu

Huwa tunahitaji watu watuchukulie kwa namna fulani, wakati huo hatutaki hao watu wajue sisi tunahitaji nini na namna gani tutaweza kupata hicho kitu. Kabla ya kufikiri kwamba watu wanajua jambo fulani, kitu cha kwanza anza wewe kutoa hoja yako ili upate mrejesho wa mada hiyo.

4. Acha kulazimisha

Tungependa kukubaliana na watu wengine, mara nyingi tunapambana kuonyesha kwa kiasi gani sisi tuko sahihi. Jaribu kutafuta eneo ambalo mnaweza kukubaliana ninyi wote ili kupata matokeo makubwa zaidi.

Msemo wa kitaaluma

Steven Covey, mwandishi wa kitabu cha tabia saba za watu wenye utekelezaji mkubwa anaemia ” Tafuta kwanza kuelewa, ili uweze kueleweka” katika mawasiliano yoyote hakikisha unaelewa kwanza kabla hujaanza kujaribu watu wakuelewe.

Je kuna namna ambavyo unataka kuongeza uelewa wako wa kuwasiliana? Je unahitaji kufanya nini kuweza kupata matokeo mazuri katika mawasiliano yako na watu?  Je utajuaje kana kwamba umefanikiwa unapowasiliana na watu?

Hayo ni moja ya maswali ambayo unahitaji kuyafanyia kazi, ili kuongeza ufanisi katika mawasaliano yako na watu wengine kazini, kwenye biashara na hata maisha binafsi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents