Burudani

‘Nammiss sana Mangwair’, asema TID, walikuwa waanzishe kipindi cha TV

TID anasema anammiss kupita kiasi swahiba wake, marehemu Albert Mangwea aka Ngwair.

DSC_7508

TID ameiambia Bongo5 kuwa Ngwair alikuwa na msaada mkubwa kwenye muziki wake.

“Unajua kukosekana kwa Ngwair kwangu ni pengo ambalo siwezi kulisahau kabisa,” amesema muimbaji huyo. “Unajua ua Ngwair kuna ngoma tulikuwa tunafanya wote na msaada wake nilikuwa nauhitaji sana maana touch zake zilikuwa nzito. Kama nyimbo zangu ‘Kiuno’,’Raha’,’Check Me’, zote hizo ameandika yeye Ngwair. Ukiacha hizo tulikuwa tunataka kuja na kipindi cha TV, kufanya movie ya Girlfriend Part 2. Vitu vyote hivyo ni mtu ambaye tulikuwa tumeanza naye. Leo unaona hayupo najiona nipo mpweke sana, maana ni mtu ambaye alikuwa akinipa idea, aisee nammiss sana,” ameongeza TID.

Kwa upande mwingine TID amezungumzia uhusiano wake na Dully kutokana na taarifa za hivi karibuni kuwa walizinguana.

“Mimi na Dully hatuna tofauti tu ni chalenji tu na juzi Dully alikuja home tuakenda studio tumerekodi ngoma ya pamoja. Kwahiyo sisi tunafanya chalenji ili tufanye kitu kizuri. Dully ni kama brother wangu amenipita mimi kama mwaka mmoja na mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanza kumtambulisha Dully stejin pale Bills enzi hizo miye nilikuwa MC wa hapo.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents