BurudaniVideos

Najutia kuwahi kuwa video queen, napenda kuimba zaidi – Lulu Diva

Kama kuna ukurasa katika kitabu cha maisha ya Lulu Diva ambao angeweza kuufuta, ni ule wa kufanya kazi kama mrembo kwenye video za Bongo Flava.

Lulu ameiambia Bongo5 kuwa anajuta kufanya kazi hiyo.

“Kama kuna kitu ambacho najutia kukifanya, ni video vixen,” amesema. “Kitu ambacho mpaka kesho ukiniuliza katika industry ya entertainment ambacho unajuta kukifanya ni nini, mimi sijajutia kuwa miss, lakini video vixen najutia kwasababu wale wanaofanya ile kazi wanajidhalilisha sana, yaani wanajiweka hawana thamani, wanajitoa thamani yao. Kwahiyo hata kama wewe utakuwa unajiweka tofauti, sababu wenzako washafanya hivyo na samaki mmoja akioza ni wote, mnaonekana wote mko hivyo,” ameongeza.

Nilipomuuliza kama akilipwa fedha nyingi kuonekana kwenye video, jibu lake lilikuwa ni, “Siwezi kukubali, sasa hivi mimi naconcentrate na muziki wangu.”

Lulu ataachia kazi yake mpya, Usimwache Jumamosi hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents