Burudani

Nahreel azidi kuwavuta wasanii wa kimataifa, Da L.E.S wa Afrika Kusini na Elani wa Kenya wataka kufanya naye kazi

Producer wa The Industry , Nahreel anazidi kupata maombi kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Afrika ambao wanataka awatengenezee midundo.

Nahreel

Baada ya K.O na AKA wa Afrika Kusini kuomba kufanya naye kazi, producer huyo mshindi wa tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Bongo Flava kwenye KTMA 2015, amesema amepokea maombi kutoka kwa wasanii wengine.

Nahreel amesema kuwa siku ya jana ametafutwa na Da L.E.S, ambaye ni rapper mwingine wa Afrika Kusini pamoja na kundi la Elani kutoka nchini Kenya, wote wakihitaji huduma yake ya midundo.

“Nimepata sana mawasiliano na wasanii wengi saivi, jana tu nimepata mawasiliano na Da L.E.S, pia anataka nimtengenezee midundo, Elani wamenicheki pia jana jana wanataka wafanye kazi na mimi, kwahiyo inaonesha ni jinsi gani recognition yangu imeanza kuonekana sehemu kubwa, na namshukuru Mungu inanipa nguvu ya kuongeza nguvu katika kazi yangu.” Nahreel aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents