Burudani

Nahreel aanzisha darasa la utengezaji wa beat

Beatmaker mahiri nchini aliyewahi kutengeneza midundo kadhaa ukiwemo Stimu Zimelipiwa (Copy my Motion) wa Joh Makini, Nahreel ameamua kukitumia kipaji chake na elimu masuala ya production kwa kuanzisha darasa la utengenezaji wa beat.

Amesema darasa hilo litajumuisha mafunzo ya kutengeneza beat, kumaster pamoja na kumix.

Akiongea ba Bongo5 asubuhi hii, producer huyo amesema darasa lake litakuwa kwenye studio ya Hometown iliyo nyuma ya Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Nahreel ameongeza kuwa mpaka sasa ana wanafunzi wanne huku mipango ya kuwa na darasa kubwa ikiwepo lakini baada ya kuona muitikio wa vijana katika kujiunga na darasa lake unaridhisha.

Mafunzo hayo yanagharimu shilingi laki mbili kwa miezi miwili.

“Watu wengi wamesikia ladha yangu tayari na wanajua utofauti huo nadhani watu wengi wanaokuja kwangu wataelewa kabisa okay kwa Nahreel tunaenda pale tunaenda kufuata muziki fulani, tunataka tujue jamaa anawezaje kufanya muziki kama huo. Kwahiyo ndio hivyo mtu akija akijiunga atapata vitu vipya,” amesema Nahreel.

Akiwa na miaka 14 mwaka 2003, baba yake alimnunulia keyboard aina ya Yamaha (350 PSR) na kumpa mwalimu ambaye alimfundisha kwa mwaka mmoja ili ajifunze kupiga nyimbo za gospel kutokana familia yao kuwa ya kisabato ambao hupenda kuabudu.

Mwaka 2005 kwa takriban miezi sita alijifunza kutumia software maarufu ya kutengeneza beat Fruity loops 3 (FL) na hivyo alichanganya ujuzi wa keyboard na FL kutengeneza beat nyumbani mpaka alipomaliza high school.

Mwaka 2007 alienda kwenye studio ya `Kama Kawa` iliyokuwa chini ya G-Solo ambaye alivutiwa na uwezo wake na kumuomba afanye kazi hapo.

Alifanya kazi kwa miezi minne na ndipo alipolazimika kwenda kusoma nchini India lakini tayari jina lake lilikuwa kubwa nchini kwakuwa alitengeneza hits za wasanii Joh Makini, Nakaya, Kala Jeremiah, Roma, Llevo , Izzo B na wengine.

Baada ya kumaliza masomo na kurudi nyumbani, Nahreel amejiunga na vijana wengine watatu kuunda kundi liitwalo PahOne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents