Michezo

Nahodha na kocha wa zamani wa Liverpool afariki

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool na nahodha ambaye pia aliwahi kuwa kocha Ronnie Moran amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, Moran alichezea klabu hiyo mechi 379 kati ya mwaka 1952 na 1966.

Alikuwa mfanyakazi aliyehudumia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi alipostaafu 1999.

Alijiunga na benchi la wakufunzi Liverpool mwaka 1966 na mara mbili alihudumu kama meneja wa muda – baada ya Kenny Dalglish kujiuzulu 1991 na Graeme Souness alipofanyiwa upasuaji wa moyo 1992.


Moran akiongoza Liverpool fainali ya Kombe la FA 1992 walipowashinda Sunderland Wembley

Mwanawe wa kiume amethibitisha kwamba alifariki mapema Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Alihudumu chini ya mameneja tisa tofauti alipokuwa benchi la kiufundi.


Ronnie Moran (kulia) na Gerry Byrne wakisherehekea kushinda kikombe cha ubingwa wa ligi dhidi ya Arsenal 1964

Aliwaongoza Liverpool fainali ya Kombe la FA wanjani Wembley mwaka 1992 akiwa meneja wa muda meneja wao Souness alipokuwa anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents