Burudani

Mzuka wa #TZW2015 waanza kutawala mitandao ya kijamii

Hashtag maalum kwa Tuzo za Watu mwaka huu ni #TWZ2015 na kama tayari umeishaitafuta, bila shaka utakuwa umekutana na picha nyingi zinazohusiana na tuzo za mwaka huu.

tzw2015_logo (1)

Msimu mpya wa tuzo za watu umezinduliwa Alhamis hii na tayari Instagram, Twitter na Facebook zimeshaanza kuchafuka kwa shamrashamra.

Mashabiki wameanza kupendekeza majina ya mastaa wao, mastaa nao wameanza kuwahimiza mashabiki kufanya kweli. Mwananchi ana rungu lenye nguvu ya asilimia 100 katika kumpata mshindi wa tuzo za watu.

Mwenye kura nyingi ndiye mshindi. Sisi tumemwekea tu shabiki vigezo lakini uamuzi upo mikononi mwake. Mwaka huu kuna jumla ya vipengele 14… yeeiiiii vipengele vimeongezeka zaidi.

Fanya kweli sasa kwa kupendekeza majina kwa njia ya website ambayo ni tuzozetu.com na njia ya sms kwa kutuma neno TUZO kwenda 15678 upate menu kama ilivyo hapo chini. Andika code ya kipengele husika, jina la unayempendekeza na kisha tuma kwenda namba 15678

1. Mtangazaji wa redio anayependwa (TZW1)
2. Kipindi cha redio kinachopendwa (TZW2)
3. Mtangazaji wa kipindi cha runinga anayependwa (TZW3),
4.Kipindi cha runinga kinachopendwa (TZW4),
5. Tovuti/Blogu inayopendwa (TZW5)
6. Muongozaji wa video za Muziki anayependwa (TZW6)
7. Muongozaji filamu anayependwa (TZW7)
8. Mwigizaji wa kike anayependwa (TZW8),
9. Mwigizaji wa kiume anayependwa (TZW9)
10. Mwanamuziki wa kike anayependwa (TZW10)
11. Mwanamuziki wa kiume anayependwa (TZW11)
12. Filamu inayopendwa (TZW12)
13. Video ya Muziki inayopendwa (TZW13)
14. Mfadhili maarufu (TZW14)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents