Habari

Mzee Yusuf na Khadija Kopa kunogesha tamasha la ‘Mitikisiko ya Pwani’ Tanga leo

Mzee Yusuf na bendi yake ya Jahazi Modern Taarab na Khadija Omar Kopa wanatarajia kutumbuiza kwenye tamasha la ‘Mitikisiko ya Pwani’ litakayofanyika Jumamosi hii (November 23) mjini Tanga. Tamasha la Mitikisiko ya Pwani 2013 limeandaliwa na kituo cha radio cha Times FM 100.5.

1456502_578568272222437_1110521339_n

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa tamasha hilo la kila mwaka kufanyika Tanga ambapo miaka iliyopita lilikuwa likifanyika jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani pekee. Miamba hiyo ya Taarab itakutana na bendi maarufu jijini Tanga ‘Kimbeji Modern Taarab’, ambayo imekuwa mahiri mkoani Tanga kutokana na uwezo wa waimbaji na wapigaji wa ala.

Mratibu wa tamasha hilo, Mzee Chapuo wa Times FM, amesema nia na madhumuni ya kupeleka tamasha hilo Tanga ni kukuza wigo wa tamasha la taarab ili liweze kufanyika katika miji mbalimbali Tanzania.

“Ni dhahiri kwamba tupo katika msimu wa Nyumbani ni Nyumbani ambapo tumetilia maanani kwamba Tanga ni nyumbani katika Taarab na ndilo chimbuko la Modern Taarab na ndio sababu tumelipeleka Tanga kwa awali. Lakini tunategemea baadae kulipeleka mikoa mingine ya Tanzania na hata nje ya Tanzania kama Mombasa Kenya,” amesema Mzee Chapuo.

Mratibu huyo ameeleza pia sababu ya kuwakutanisha mfalme na malkia wa taarab katika tamasha hilo.

“Sababu kubwa ya kuwapeleka Mzee Yusuf na Khadija Kopa ni kwa sababu ni viongozi wa bendi ambazo zimekuwa bingwa katika fani hiyo ya modern taarab, pili palipokuwa na mfalme malkia huwa anakuwepo. Na ndio maana tumeamuwa kuwapelekea wakazi wa Tanga Mfalme na Malkia wa Mipasho,” amesema Mzee Chapuo.

Source: Timesfmwebsite

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents