Habari

Mzee Small aendelea vizuri baada ya kupatwa na Kiharusi

Msanii mkongwe katika tasnia ya sanaa ya maigizo na vichekesho nchini maarufu kama Mzee Small ameongea na bongo5 exclusively na kusema kwa sasa anaendelea vizuri kiasi japokuwa hali yake bado haijatengemaa kwa asilimia kubwa.

Tukimnukuu anasema “mimi bado naumwa na ugonjwa wa “kiharusi” ambapo tangu tarehe 20 mwezi 5 mwaka huu mpaka leo hii kidogo nimekuwa napatiwa matibabu kwa matabibu wa tiba asilia. Ugonjwa huu niliupata wakati natokea Mwanza ambapo nilikuwa nimechukuliwa na mtangazaji mmoja, jina silikumbuki na kuwaburudisha kabla ya kusafiri kwenda nje ya nchi.

Ugonjwa huu ulinipata asubuhi ya tarehe hiyo tano baada ya kurudi kutoka Mwanza ambapo baada ya kulala nilipoamka nikajikuta mwili unagoma kufanya matendo ya kawaida yaliyozoeleka kama kushindwa kuamka na kukaa kwenye kiti mwenyewe bila msaada wa mtu mwingine.

Kuona hivyo mke wangu akanipeleka kwenye moja ya hospitali ya maeneo ya hapa Tabata Kimanga, ndipo walipogundua nina Kiharusi na daktari akanieleza nimepooza upande wote wa kushoto kwangu.”

Mzee Small anaendelea kusema baada ya matibabu ya awali wauguzi na madaktari walimhamishia hospitali ya taifa Muhimbili ingawaje kwa sasa anadai anamtegemea zaidi tabibu wa tiba asilia kutoka Kigoma ambaye ndiye anafanya kazi ya kumitibu kwa kumchua, kumnyoosha na kumfanyisha mazoezi ya viungo.

Mzee Small alichukua fursa hiyo ya kuongea na bongo5 kuwashukuru wadau wote wakiwemo wasanii ,vyombo vya habari, ndugu jamaa na marafiki kwa kuweza kumchangia kwa namna moja na nyingine pamoja na kupigiwa simu na watu wengi wa kumtakia kheri.

Alimalizia kwa kuwashukuru wananchi wote kwa kumjali katika kipindi hiki kiugumu kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents