Bongo Movie

Mzee Chilo adai ugomvi wa Bongo Movie Unity unatokana na uchu wa madaraka

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Mzee Chilo amesema ungomvi unaotokea ndani ya Bongo Movie Unity unasababishwa na uchu wa madaraka.

Mzee Chilo akizungumza jambo na watoto

Chilo amesema hakuna chochote kinachogombaniwa zaidi ya madaraka ndani ya tasnia hiyo ambayo amedai imekosa ushirikiano.

“Nimesikia mengi sana kuhusu bongo movie unity, sijui huyu kajiuzulu lakini niseme ukweli tatizo ni uchu wa madaraka,” ameiambia Bongo5. “Kila mtu anamwona mwenzake anakula sana, sasa kwa hali hii hatuwezi fika kokote. Sisi ni wamoja bila kuwa na taasisi za kutuongoza tutaishi vipi? Mimi hawakutaka ushauri wangu kuhusu hili suala ndio maana wala sikuliingilia, wakinihitaji nitawashauri. Kikubwa cha kuwashauri nawataka tushirikiane, tuache tofauti zetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents