BurudaniVideos

Mwasiti, Shilole na Queen Darleen waeleza kwanini wameanzisha kampeni ya ‘Sisters’ (Video)

Urafiki wao umesababisha kuanzishwa kwa kampeni ya ‘Sisters’ Binti wa Leo, Mwanamke wa Kesho.

12935101_1693011684286484_1147151154_n

Mwasiti ameiambia Bongo5 kuwa Sisters ina wasichana/wanawake sita wakiwemo yeye, Shilole, Queen Darleen, Linah, Kajala.
Amedai kuwa mara nyingi huwa pamoja na wanafahamiana ndani na nje na hivyo waliona ni vyema urafiki huo ukazalisha kitu cha msingi kitakachowasaidia wasichana wengine.

Kwa upande wake Shilole amesema anapenda kutumia kampeni hiyo kuelezea historia yake na jinsi ambavyo maisha yake yaliharibika akiwa binti baada ya kudanganywa na wanaume.

“Kwahiyo ndio tukasema tuseme na wale mabinti ambao ndio kwanza watakuja kuwa wanawake wa baadaye, tuwaambie kwamba sisi dada zenu ambao tulikimbilia hayo maisha ya juu yametuponza kiasi gani, wa kwanza mimi hebu tujifunze kupitia Shilole,” amesema.

Kwa sasa Sisters wanapita kwenye shule za Dar es Salaam kuzungumza na wanafunzi wa kike na kuwashauri jinsi ya kujikita kwenye elimu kuandaa mustakabali unaofaa.

Mwasiti amesema wanatarajia kwenda katika shule sita katika kila mkoa nchini. Amesema Sisters Movement ina watu wengine ambao ni wataalam wa masuala mbalimbali ya kijamii kama wanasaikolojia, madaktari, wanasiasa na wengine ambao huzungumza na wanafunzi.

Kwa upande wake Queen Darleem amesema wanataka kutumia kampeni hiyo kuwapa wasichana wa leo kile walichokikosa wao wakati wakiwa mabinti kiasi cha kujikuta wakiingia kwenye maisha makubwa kabla ya wakati.

“Mwisho wa siku sisi ndiyo inabidi tuanze kuongea nao, ambao tayari yameshatukuta, wazazi wetu hawakupata nafasi ya kuongea na sisi,” anasema Darleen. “Tumekuja kupata tatizo ndiyo wamekaa chini kuongea na sisi. Kwahiyo sasa hivi sisi tunajaribu kuongea na hao wanafunzi wajue kwamba kitu gani kibaya,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents