Burudani

Mwasiti na Banana Zorro wateuliwa mabalozi wa kampeni ya ‘Stand Up For African Mothers’

Mwasiti na Banana Zorro wametangazwa kama mabalozi wa kampeni ya ‘Stand Up For African Mothers’

Msanii Maarufu wa Kizazi Kipya Mwasiti( Kulia) ametangazwa kama Balozi wa kampeni ya Stand Up For African Mothers, akiongea na waandishi wa habari
Mwasiti akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangazwa kama mmoja wa mabalozi wa kampeni ya Stand Up For African Mothers

Mwasiti ameiambia Bongo5 kuwa amesema amefurahi kuchaguliwa kuwa balozi. “Unajua hii inaonyesha jinsi gani sasa hivi wasanii tunathaminiwa. Tutakuwa mabalozi wa hii kampeni kwa muda wa mwaka mmoja na pia tutazunguka Tanzania nzima kutoa elimu,” amesema.

Wanawake 7,900 wa Tanzania hupoteza maisha kila mwaka wakati wa kujifungua. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo hivi vingeweza kuepukika endapo wahudumu wa afya wenye utaalamu wangetoa huduma kwa wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua. Kwa kuamini kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank za Barclays na Bank M wameonesha nia ya kuongeza nguvu na juhudi za kutunisha mfuko wa kusaidia mafunzo ya wakunga kupitia kampeni yake ya Stand up for African Mothers.

Msanii maarufu wa kizazi kipya Banan Zoro  ametangazwa pia kuwa balozi wa Kampeni hii ya Stand Up for African Mothers inayoendeshwa na Amref kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi
Banana Zorro alipokuwa akitangazwa kuwa balozi wa kampeni ya Stand Up for African Mothers

Kampeni hiyo ya kimataifa inalenga katika kuongeza uelewa juu ya mchango unaotolewa na wakunga wenye ujuzi katika kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga. Kampeni hii pia inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakunga 15,000 katika nchi 13 za Afrika, kati yao wakunga 3800 wanatarajiwa kupata mafunzo nchini Tanzania ifikapo mwaka 2015/2016. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Changia mafunzo ya wakunga , okoa maisha ya mama na mtoto” kwa kuunga mkono nia hii njema unasaidia kuwapatia mafunzo wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto nchini Tanzania.

maxresdefault

Nchini Tanzania kampeni hii ilizinduliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 15 Mei mwaka 2012. Mke wa Raisi amekuwa balozi wa kampeni hii akiongoza juhudi za kuwaokoa kina mama wa kiafrika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents