Burudani

Mwasiti azungumzia tetesi za ujauzito na ujio wa ngoma mpya

Muimbaji anayefanya vizuri na wimbo wa Serebuka, Mwasiti ameshangazwa na watu wanaomzushia kuwa ni mjamzito na kukanusha japo amedai anatamani kuwa na mtoto.

10533297_1446091095676792_378714490_n

Akizungumza na Bongo5 leo, Mwasiti amesema hana mpango wa kuolewa kwa sasa na wala hana ujauzito kama watu wanavyozusha. “Nasikia eti watu waniambia nina mimba, sina mimi na sijui hizo habari watu wanazipata wapi,” amesema. “Sina mpango wa kuolewa, vyote watu wanazusha tu. Kweli hakuna mwanamke asiyetamani kuwa na mtoto hata mimi napenda sema ni majaliwa, mambo yote anapanga Mungu,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Mwasiti amezungumzia ujio wa wimbo yake mpya uitwao ‘Leo’ aliomshirikisha Godzilla.

“Nina ngoma mbili ambazo ninategemea ziende mtaani. Nina Leo ambayo nimemshirikisha Godzilla halafu nina Kisigino ambayo nimeimba mimi peke yangu lakini sijajua itatoka ipi, Nyimbo zote mbili ni aina mbili tofauti za muziki. Muziki wa Mwasiti wa sasa hivi upo kwelI leo, lakini kwenye Leo tumeimba tofauti, mtashangaa kumuona Godzilla ambaye amebadilika sio Godzilla ambaye amezoeleka, ni Godzilla mwingine kabisa, nimeamua kumbadilisha.”

“Kwahiyo ukisikiliza Leo utasikiliza ladha mbili tofauti, utamsikia Godzilla na Mwasiti. Hiyo tumefanya chini ya producer Chizan Brain, B Records na Kisigino ni wimbo wa kuchezeka na tumefanya na Shebby Records. Kwahiyo yoyote kati ya hizo inaweza ikatoka lakini itaanza video kwanza.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents