Burudani

Mwasiti asimulia mazingira magumu yaliyopo kwenye shule za vijijini ‘hali ni mbaya jamani’

Muimbaji wa ‘Serebuka’ Mwasiti amedai kuwa anasikitishwa mno na ukweli kuwa wanafunzi wengi wa shule za msingi nchini hawana madawati na bado wanakalia mawe.

10953589_343631809156356_735313203_n

Mwasiti amesema hivi karibuni amekuwa akizunguka katika mikoa mbalimbali kutembelea shule katika majukumu yake ya kampeni za elimu.
“Hali ni mbaya jamani,” amesema Mwasiti.

926565_475340189271641_598014993_n
Mwanafunzi anayesoma katika moja ya shule za msingi nchini

“Unajua sio vijijini tu hata mijini ikiwemo kwa baadhi ya shule hata hapa jijini Dar es Salaam, huwezi amini mpaka naongea na wewe watoto bado wanakalia mawe, vyoo hakuna vya kutosha, vitendea kazi hakuna watoto wanasoma katika mazingira magumu na mabaya. Vilevile hata watoto walemavu wapo shule lakini hawana facilities kuwa sawa na watoto wengine wengine, wanatumia mikono kutembelea na wanaenda chooni jamani,” amesema Mwasiti.

Tayari ameshaitembelea mikoa ya Kigoma, Mwanza na Mara.

“Nitazunguka kutoa madawati katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara ambapo nilifanya hivyo mwaka juzi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara na kufikia Februari Mosi nitakuwa nimeshajua ratiba yangu nianzie mkoa gani.”

Chanzo: Bomba Base Show, Bomba FM Mbeya

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents