Tragedy

Mwanamuziki na mbunge wa Somalia Saado Ali auawa

Mwanamuziki maarufu ambaye pia ni mbunge nchini Somalia, Saado Ali Warsame amepigwa risasi na kufa na wanamgambo. Aliuawa pamoja na mlinzi wake, katika shambulio la kutumia gari mjini Mogadishu.

rr
Msemaji wa kundi la al-Shabaab, Abdulaziz Abu Musab ameiambia BBC kuwa ameshambuliwa kutokana na sababu za kisiasa na sio muziki wake.

Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu Mohammed Moalimu amesema huyu ni mbunge wa nne kuuawa mwaka huu. Bi Warsame alipata umaarufu enzi za utawala wa rais wa zamani Siad Barre, aliyeondolewa madarakani mwaka 1991.

Aliishi uhamishoni nchini Marekani kwa muda mrefu na alirejea mwaka 2012 na kuwakilisha ukoo wake katika bunge jipya la Somalia. Mwandishi wa BBC Idhaa ya Kisomali Abdullahi Abdi anasema Bi Warsame atakumbukwa zaidi kwa muziki wake.

Alikuwa mmoja wa wasomali wanawake wachache aliyepanda jukwaani bila kujifunika kichwa na mara nyingine kuvaa suruali, jambo ambalo sio la kawaida kwa wanawake wa Somalia, amesema Abdi.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents