Habari

Mwanaanga wa mwisho kufika mwezini Eugene Cernan afariki dunia

Eugene Cernan ambaye alikuwa mtu wa mwisho kufika mwezini Disemba 1972 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya marehemu, Eugene amefariki Jumatatu hii kutokana na matatizo za afya japo hawajaweka wazi zaidi ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Eugene amekuwa ni mmoja kati ya wanaanga 12 waliowahi kufika mwezini akiwa tayari amewahi kufika takribani mara tatu ikiwemo mwaka 1966, 1969 na 1972 kabla ya kustaafu mwaka 1976 katika shirika la NASA.

Kifo cha Cernan kimetokea zikiwa zimepita wiki chache tangu kilipotokea kifo cha mwanaanga mwingine wa NASA, John Glenn aliyefariki Disemba 8, mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents