Diamond Platnumz

Mwana FA, Stamina, Diamond, Mwasiti na wengine 6 warekodi wimbo kuhamasisha matokeo mazuri shuleni ‘Tokomeza Zero’

Linex, Roma, Lina, Mwana FA, Mwasiti, Stamina, Diamond, Maunda Zorro, Peter Msechu, Keisha na Kala Jeremiah wamerekodi wimbo uitwao ‘Tokomeza Zero’ kuhamasisha matokea mazuri shuleni.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/106147791″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Wimbo huo umeandikwa na Lameck Ditto na kutayarishwa na Tudd Thomas kwenye studio yake, Tudd Thomas Production.

Akiongea na Bongo5, Mwasiti amesema wimbo huo umeandikwa kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi kuipenda shule.

“Hatutaki sifuri, tunataka usome, ukija kwenye sekta yoyote kufanya kazi uwe na elimu yako,” amesema.

“Na ndio maana kama umeona Tokomeza Zero ina wanamuziki wenye majina makubwa akina Diamond. Wana tamani kurudi shule. Wanaujua uchungu wa shule, kuna akina Mwana FA, akina Lina akina Roma.”

Msikilize zaidi hapa;

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/106148633″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents