Burudani

Mwana FA kutumbuiza kwa mara ya kwanza kwenye Fiesta mwaka huu mjini Singida

Baada ya kupagawisha wananchi wa Mbeya na shoo kali mwishoni mwa wiki iliyopita, tamasha la Serengeti Fiesta 2014 linaelekea Singida kukata kiu ya mashabiki wake ambao walikuwa wakilisubiri kwa hamu.

mwana fa

Shoo hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imepangwa kufanyika hapo October 3, katika uwanja wa Namfua.
Wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Mwana FA, Nikki II, Makomando, Stamina, Ney, Young Killa, Linah, Recho, Mr. Blue, Dully Sykes, Mo Music na Baraka Da Prince.

Mwana FA atatumbiza kwa mara ya kwanza katika shoo za tamasha la hilo mwaka huu mjini humo.

“Nimefarijika kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza mjini Singida na ningependa kuwashauri mashabiki wangu waje kwa wingi kunishuhudia jukwaani nikifanya mambo wakati wa shoo,” alisema.

Kabla ya shoo hiyo, kutakuwa na shughuli nyingine mbalimbali kama shindano la Serengeti Super Nyota Diva ambalo mshindi atajinyakulia tiketi kwenda kushuhudia shoo ya mwisho ya tamasha hilo litakayofanyika hapo Oktoba 18, 2014 jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents