Burudani

Mwana FA kuangusha bonge la shoo nyumbani Tanga

Wakazi wa Tanga wametakiwa kukaa mkao wa kula kwani burudani ya nguvu ya muziki itapigwa moja kwa moja jukwaani siku ya tarehe 31 ya mwezi huu wa Oktoba katika ukumbi wa Lasachika mkoani humo.

001.MWANAFA TANGA
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati alipokuwa akizungumzia kuhusiana na shoo ya”Vodacom life is better”itakayofanywa na msanii wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA (kushoto)siku ya ijumaa katika klabu ya La Casachika mjini Tanga.Kulia ni Meneja wa msanii huyo Lusajo Mwaisaka

Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya Mashariki kwa vibao vyake mbalimbali si mwingine ni MwanaFA.

FA atafanya shoo laivu mkoani Tanga chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania akisindikizwa na DJ Zero pamoja na mtangazaji wa Clouds FM B12.

Rapper huyo mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki wa kizazi kipya nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki nchini.

Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Tanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema Vodacom Tanzania wakiwa kama wadau namba moja wakuu wa kuinua tasnia hii ya muziki na michezo kwa ujumla wameamua kudhamini shoo ya “Vodacom Life is better”itayofanywa na Mwana FA mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wao, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru kwa kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo.

“Hivyo ndivyo Vodacom tunafanya maisha ya wateja wetu kuwa murua,”alisema Mworia.

“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini,” aliongeza.

Kwa kuongezea Mworia amewaomba wakazi na mashabiki wote wa MwanaFA na muziki wa Hip Hop kujitokeza kwa wingi katika shoo hiyo iliyopewa jina la”Vodacom life is better show”kwani mbali na burudani kuwepo kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom. “Hivi ndivyo ambavyo Vodacom tunafanya maisha ya wateja wetu kuwa murua,” alisisitiza Mworia.

Naye MwanaFA alisema kwamba katika kunogesha shoo yake hiyo ameamua kuambatana na DJ Zero ambaye atakuwa akifanya mambo yote kwenye jukwaa kwani ni mkali na anaijua kazi yake. “Shoo hiyo si ya kukosa kabisa kwani nimejipanga vya kutosha kuwaburudisha ndugu zangu wa nyumbani kwa hiyo uwepo wako tu pale utakufanya ujisikie vizuri kwani nitatenda haki kwenye shoo hiyo. Nawapenda sana wakazi wa Tanga na nipo tayari kuwaburudisha kama nifanyavyo sehemu zingine ndani na nje ya nchi,” alisema Mwana FA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents