Burudani

Mwana FA aeleza kwanini video nyingi za waongozaji wa Bongo hazichezwi nje

Rapper Hamisi Mwinjuma aka Mwana FA ambaye alishoot video ya hit yake, Mfalme nchini Kenya, ameeleza sababu anazohisi zinachangia video zinazoongozwa na waongozaji wa Tanzania kushindwa kuchezwa kwenye vituo vya runinga vikubwa vya nje.

mwana fa

Mwana FA amesema sababu kubwa ni kukosekana kwa connections.

“Kinachokosema kwa directors wetu ni large connection,” FA aliiambia EFM jana. “Nafikiri wanafanya video vizuri. Kuna wakati Adam Juma alikuwa ana video kuliko directors wote wa Africa kwenye Channel O, alikuwa ana video nyingi zaidi kuliko madirector wote, by 2005, 2006. Lakini baadae ikawa imeyumba, nafikiri connection ikapotea kama hivyo,” ameongeza Mwana FA.

“Kuna madirector wa Nigeria na director wa Kenya wanaweza wakafikisha muziki wetu sehemu, lakini ukiangalia nyimbo za madirector wa Tanzania zilizofika huko kwa miaka 2,3 iliyopita utakuta ni sifuri. Niambie video ya director wa Tanzania ambayo imepigwa Trace! Sio kwamba wanatengeneza nyimbo mbaya, niseme kwamba nafikiri hatujafikia kile kiwango cha kujua nini kinatakiwa kifanyike kwenye kufikisha video. Nawaza kwamba kitu ambacho kinaniumiza kichwa kila siku ni namna ambavyo industry inavyokuwa, haitakiwi kukuwa wasanii peke yao. Wanatakiwa kukua wasanii, wanatakiwa kukua mameneja, maproducer na video directors, yaani inatakiwa tukuwe kama industry. Huwezi kuwa na wasanii wakubwa halafu hauna producers bora au madirector wazuri nchini au hamna mameneja wazuri, tutakuwa tunapoteza nafasi zetu. Hatuwezi tukawa tunatoa dola elfu ishirini kila siku kuwapelekea akina Moe Musa, akina Godfather wakati hata wakati mwingine tunaweza kukafanya video kama hiyo kwa dola elfu kumi kwa Adam Juma ama less ya hapo.”

“Kwahiyo kama industry, inabidi tukuwe, video zifanyiwe hapa ili watu wengine wa nje wawe wanaleta video zao zifanyiwe hapa kwa madirector wa kibongo ili mzunguko wa hela uwe unaendelea lakini wakati huu wakati wanajaribu kufikira nini wanatakiwa wakifanye, sisi inatubidi tusisimame kungoja kwamba mpaka wao wakue ndo tufanye video,Inabidi tuendelee kufanya huko ambako watu wamekuwa, kwamba watu wana connection, network iko vizuri ili tuweze kuonekana kwa upana mkubwa zaidi Afrika nzima. IkifIka tutabebana huko mbele ya safari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents