Burudani

Mwana FA aeleza kilichomvuta kwenye mazoezi ya boxing na kujenga mwili, asema mazoezi yamemfanya awe na adabu

Ukikutana na Hamis Mwinjuma aka Mwana FA, si yule uliyemuona miaka minne au mitatu iliyopita. Huyu wa sasa amejaza na amepasuka kama bondia.

10665468_504286639719417_1437979274_n

FA amezungumza na Bongo5 kuhusu kipi kilichomfanya aanze kufanya mazoezi hayo na namna yalivyombadilisha kitabia na kimwili.
“Mazoezi unajua ni mateso bila sababu, yaani hujakosa kitu chochote lakini unapewa adhabu,” amesema FA.

“Kwahiyo inabidi uwe dedicated kweli kweli kwamba unaumia lakini unaenda kuna kitu kingine unakiwaza zaidi ya maumivu yaani you feel past your pain.”

11356757_771070109675723_2010033393_n

FA anasema sababu ya kuanza kufanya mazoezi ni ushawishi kutoka kwa bondia, Japhet Kaseba. Pia ni kutokana na kuwa shabiki wa michezo ya ngumi kwa muda mrefu.

“Napenda jamaa wanavyofanya fitness na nafurahia wasanii wakiwa na miili mizuri kwasababu yenyewe pia ni moja ya sehemu ya muziki wao, yaani ipo kwenye package, muonekano,” ameongeza.

FA anasema anafahamiana na Kaseba kitambo kwakuwa walikuwa wakiishi mtaa mmoja maeneo ya Upanga. Aliwasiliana na Kaseba aliyempa ujumbe kupitia kwa AY na kuanza kwenda kwenye gym yake ambapo alipewa mtu wa kumuongoza.

11176596_1390016944656752_1662334961_n

“Kwanza kabidsa nimeenda, [Kaseba] akanipa jamaa ni mwanajeshi, kapteni wa timu ya taifa ndio akawa ananitrain,” anasema FA.
Anasema aliongezewa trainer mwingine aliyemtaja kwa jina la Khalifa ambapo wawili hao ni wajuzi wa boxing na kick-boxing.

“Wale jamaa ukikaa nao, wanakupa moto hivi,” anasema.

“Kila siku unakuwa unajiona ‘ebana mimi siwezi’ na vyovyote unavyofanya wewe mazoezi yako yako chini kidogo, ‘huyu afanye mpaka hapa’, halafu unaona wenzio wanafanya zaidi. Na ukienda pale kwa Kaseba unakuta vijana tu wengine hawana hata kazi lakini mazoezi yao yanakutisha. Yaani naenda pale najikuta mimi ndio mtu mzembe kuliko wote, kwahiyo hiyo ikawa inanipa moto. Kuna kipindi nilikuwa natoka home Kijitonyama nakimbia mpaka kwa Kaseba Mwananyamala kabla ya kuanza mazoezi.”

Mwana FA anasema baada ya kuyazoea mazoezi, alijikuta yakimwingia kiasi cha kumfanya kuwa addicted. “Sasa hivi nisipoamka kwenda gym nasikia vibaya mwenyewe. Imefika mahali lazima nitrain siwezi kuacha.”

Rapper huyo anasema mazoezi ya mwili na boxing yamembadilisha kwa kiasi kikubwa kutoka kuwa mtu mwenye hasira za haraka hadi kuwa mvumilivu wa mambo mengi.

“Mimi nilikuwa nakasirika sana,” anasema.

“Lakini baada ya kucheza ngumu hivi naona vitu vyote vimebadilika na nimekuwa na adabu zangu vizuri,” amesema FA.

“Na sababu yangu ya msingi ni moja tu. Kuna watu hutaamini wana fitness hiyo waliyonayo ukiwaona kwasababu fitness haiandikwi usoni. Haijalishi unakasirika vipi, inabidi urudishe hasira zako chini kwasababu unaweza kukwaruzana na mtu kidogo, ukajikuta hauna meno au nini.”

“Kwa mfano kuna mchizi mmoja nilikuwa namkuta kwa Kaseba pale mpaka namuita monitor, very good boxer. Sasa mimi nilikuwa sijui kazi yake, yaani boxer mkali sana na anawakalisha watu. Siku moja naenda Zanzibar nimemkuta yule jamaa anauza korosho zake pale. Sasa imagine muuza korosha halafu umemkorofisha halafu yuko fit hivyo! Kwahiyo inakupa discipline unagundua kwamba ngumi haziandikwi usoni. Inabidi iwe kwa kujilinda mwenyewe ukikoroshwa ikibidi ujitetee ndio utazitumia ujaribu kujiokoa lakini haibidi uwe unajisifia na fitness yako.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents