Michezo

Mwamuzi Mark Clattenburg awaomba msamaha klabu ya Hull City

Mwamuzi kutoka Uingereza Mark Clattenburg ambaye hivi karibuni alitangazwa kuwa mwamuzi bora zaidi duniani, alichezesha mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza siku ya Jumamosi, February 11 kati ya Arsenal na Hull city aliwaomba msamaha wachezaji wa Hull City kwa kulikubali goli la Sanchez alilofunga kwa mkono katika dk 34 ya mchezo.

Mchezaji wa Hull city Andrew Robertson amesema kuwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza mwamuzi huyo wa kati aliwafata na kuomba msamaha kwa kosa hilo,.

“Tulipokuwa tunatoka mapumziko, mwamuzi alituomba msamaha na akasema mpira ulishikwa , kwa hiyo lazima atakuwa aliangalia tena kipindi cha mapumziko na akaona kuwa alikosea.

Ilitokea kwa haraka sana, ni vigumu mno kwa mwamuzi, lazima ujisikie hali ya huruma kwake ” Robertson aliiambia Sky Sports 1.
Katika mchezo huo Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri ,magoli yote yalifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 34 Pamoja na dakika ya 90’+3′ kwa mkwaju wa penati.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents