Burudani

Muziki wangu hauhitaji kelele nyingi – Ditto

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Lameck Ditto amesema muziki wake hauhitaji kelele nyingi kama wa wasanii wengine.

11410494_715418041918580_99643172_n

Amedai kuwa wimbo wake ‘Wapo’ hadi leo bado unamwingizia pesa nyingi kupitia miito ya simu, (RBT). Ditto ameiambia Bongo5 kuwa tangu anaanza muziki alishajua pesa ya muziki wake ataipata kwa njia gani.

“Nina namna tofauti na watu wengi wanavyofanya muziki wao,” anasema.

“Siku zote nasema niliamua kuwa hivyo kwa muziki wangu ulivyo. Toka siku ya kwanza niliamua muziki wangu uwe hivi ulivyo. Nitakuwa natoa nyimbo fulani kila baada ya muda fulani. Sipendi kujisifia nyimbo zangu zinakaa muda mrefu. Wimbo kama Wapo, Tushukuru Kwa Yote ni nyimbo mpaka leo zinafanya poa. Na katika soko mimi nyimbo zangu zinafanya vizuri kwenye ringtone, huko kwenye caller tune vizuri sana. Hazijawahi kushuka kimauzo mpaka leo,” ameongeza.

“Sasa hiyo ni ni target, soko lako ni wapi na unataka kuwauzia akina nani? Kama soko lako lipo strong mimi sidhani kama nina haja sana ya kupiga vitu mfululizo. Kila muziki na aina yake. Muziki wangu mimi hauhitaji kelele nyingi. Tuko watu tofauti na kuna wengine wana style yao. Kwa mimi naona nipo sehemu sahihi, nimechangua sehemu ambayo nimeona inafaa na ingekuwa ni mbaya ningeshaiacha. Ukiona siiachi ujue nafaidika sana kwa kiasi kikubwa,” amesisitiza Ditto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents