Habari

Muziki wa Tanzania umepenya vipi wakati tunawakilishwa na msanii mmoja tu? – Dudu Baya

Dudu Baya anapingana na kauli kuwa muziki wa Tanzania umepenya Afrika.

Dudu Baya na Mr Nice akiwa wamepozi

Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, rapper huyo amesema muziki wa Tanzania haujapenya kwakuwa anayeiwakilisha Tanzania ni mmoja tu – Diamond.

Amesema ili muziki wa Tanzania uweze kusemwa umepenya kimataifa ni lazima kuwepo na wasanii wengi wanaofanya vizuri kama ukubwa wa Diamond kwa sasa.

Amedai kuwa muziki wa Nigeria ndio uliopenya zaidi kwakuwa kuna wasanii wengi wanaofanya vizuri na wenye ukubwa sawa tofauti na Tanzania.

Rapper huyo amezitaja chuki, wivu na kubaniana ndio sababu kubwa za muziki wa Tanzania kushindwa kupenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents