Burudani

Muziki wa taarab haujafa ila mashabiki wanataka vitu vizuri – Mkubwa Fella

Meneja ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na mchango wake wa kuinua vipaji vya wanamuziki wachanga hadi kuwa maarufu, Saidi Fella ‘Mkubwa Fella’ amedai muziki wa taarab haujakufa kama baadhi ya watu wanavyodai.

Mkurugenzi huyo wa Yamoto Band ambaye ameingia kwenye muziki wa taarab kwa kuanzisha bendi ya ‘Yah TMK Taarab’ amedai hakuna ukweli wowote kwamba muziki wa taarab umekufa.

“Mimi siamini kwamba muziki wa taarab umekufa, mashabiki wapo wanazaliwa kila siku wanataka muziki mzuri,” Mkubwa Fella alikiambia kipindi cha Jahazi ya Sham Shama ya ITV.

Fella amesema yeye pamoja na bendi yake hiyo wamejipanga kuleta ushindani mpya kwenye muziki wa bendi kwa kuachia kazi nzuri.

“Ukija kwenye Yah TMK Taarab utapata kila kitu, sasa hivi tupo chimbo tunaanda kazi nzuri, kwa sababu ingawa tuna watu ambao wanamajina makubwa au wana uwezo mkubwa lakini mashabiki hawataki majina, wanataka kazi, kwahiyo sisi tumejipanga vizuri na tunakuja kutoa burudani kwa sababu mashabiki wapo wengi wanataka kazi,” alisema Fella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents