Burudani

Muongozaji wa filamu za James Bond ajitoa, ni baada ya Daniel Craig naye kudaiwa hatorejea tena kama 007

Sam Mendes, muongozaji wa filamu aliyewahi kushinda tuzo za Oscar na aliyeongoza filamu mbili za mwisho za James Bond, ‘Spectre’ na ‘Skyfall’, amejitoa kwenye mradi huo.

image

“Ilikuwa ni safari ya kuvutia, nilipenda kila sekunde yake” Mendes alisema kwenye tuzo za  Hay kwa mujibu wa gazeti la The Guardian. “Lakini nafikiri ni muda wa mtu mwingine.” “Mimi ni msimulizi,” aliongeza. “Mwisho wa siku nataka kufanya hadithi na wahusika wapya.”

Bado haijulikani iwapo nyota Daniel Craig atarejea kwenye filamu mpya ya 007 inayosimamiwa na MGM na Sony. Kuna tetesi nyingi za muigizaji yupi atachukua nafasi yake huku wanaotajwa zaidi wakiwa ni Tom Hiddleston, Idris Elba na Jamie Bell.

image

“Sio demokrasia,” alisema Craig. “Barbara Broccoli huamua nani atakuja kuwa Bond ajaye, mwisho wa story.”

Ni Broccoli, mtayarishaji mkongwe wa filamu hizo aliyemchagua Craig, ambaye kipindi hicho alikuwa hana jina na hakuna aliyekuwa akimuunga mkono.

Filamu hizo mbili za mwisho zilizotoka mwaka 2012 na 2015, ziliingiza karibu dola bilioni 2 kwenye majumba ya sinema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents