Burudani

Muigizaji mkongwe wa India Om Puri afariki dunia

Muigizaji mkongwe wa filamu za India, Om Puri amefariki dunia Ijumaa hii akiwa na umri wa miaka 66.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka zimedai kuwa Puri alifariki nyumbani kwake Mumbai baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo. Filamu ya kwanza ya Puri kuigiza ilikuwa ni Ghashiram Kotwal ambapo ilikuwa ni mwaka 1976. Lakini pia mwaka 2004 muigizaji huyo alitunukiwa nishani ya staha ya OBE kwa mchango wake katika tasnia ya filamu Uingereza.

Aliwahi kuigiza filamu kibao katika enzi za uhai wake ikiwemo ‘East is East’, ‘Mahatma Gandhi’, ‘Ardh Satya’, ‘Sadgati’, ‘Paar’, ‘Jaane Bhi Do Yaaro’ na nyingine nyingi.

Mastaa mbalimbali wa India wametuma salamu zao za rambi rambi kupitia mtandao wa Twitter wakiongozwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi.

Narendra Modi: The Prime Minister condoles the passing away of actor Om Puri & recalls his long career in theatre & films.

Akshay Kumar: Sad to hear about the passing away of the very talented Om Puri, my co-actor in many films…heartfelt condolences to the family. #RIP.

Priyanka Chopra: The end of an era …. The legacy lives on.. RIP #OmPuri.

Sachin Tendulkar : You will live in our hearts forever through the impressions you have left with your versatility. We will miss you. RIP #OmPuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents