Habari

Mugabe adai Afrika itajiondoa kwenye Umoja wa Mataifa iwapo matakwa yake hayatotimizwa

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amedaiwa kusema kuwa bara la Afrika lipo tayari kujiondoa kwenye Umoja wa Mataifa, kama matakwa yake ya kufanyika mabadiliko hayatofikiwa.

robert-mugabe-710x400

Kwa mujibu wa ripoti za Jumapili (Sept 25), Mugabe alidai kuwa Umoja wa Afrika una mpango wa kuanzisha kundi na nchi kama Urusi, China na India kama baraza la usalama la umoja huo halitowajumuisha wajumbe kutoka Afrika mwakani.

Mwanasiasa huyo mkongwe alitoa kauli hiyo wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare ambako alilakiwa na mamia ya wafuasi wa chama cha Zanu-PF akitokea kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York.

“Si wajumbe wote wa kudumu ni wagumu. Ni Uingereza, Ufaransa na Marekani. Kama wakiendelea kuwa wabishi, wasije kulalamika pindi tukikubali kuanzisha muungano wetu wenyewe na nchi kama China, India na nchi zingine za Asia. Hiki ndicho tunakitaka kufanya mwakani Septemba tutakapokubaliana,” Sauti ya Amerika ilimnukuu Mugabe.

Kauli hiyo ya Mugabe inaweza kusababisha mjadala mkubwa Afrika.

Tangu mwaka 2005, nchi za Afrika zimekuwa zikiomba ziwe na viti viwili vya kudumu kwenye baraza la usalama pamoja na vitano vya muda lengo likiwa ni kuwa na uwakilishi sawa katika chombo hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents