Michezo

Mugabe aagiza wanamichezo wa Zimbabwe walioshiriki Olimpiki wakamatwe?

Kuna habari imesambaa mtandaoni kuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi hiyo Augustine Chihuri kuwakamata wachezaji wote wa timu iliyokwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil.

Mugabe

Inasema Mugabe amechukua hatua hiyo baada ya kuumizwa na wachezaji hao kushindwa kupata hata medali moja kwenye mashindano hayo huku pesa iliyowekezwa kwenye timu ili kuiwakilisha nchi ingeweza kutumiwa kununulia dawa na kujenga shule.

“Jambo hili ni sawa na mwanaume asiyelijali kuoa wanawake watano, maana yake nini? Nitahakikisha tunagawana hasara, wote watailipa serikali bila kujali huku wakijua kuwa fedha zilizowapeleka huko zinatoka kwenye mifuko ya wananchi,” Mugabe anadaiwa kusema.

“Tumepoteza pesa za taifa kwa ajili ya hao panya tunaowaita wanamichezo. Kama hauko tayari kujitoa na kushinda japo medali ya shaba kama wenzetu wa Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda kupoteza pesa zetu,” ameongeza.

Cha kuchekesha zaidi, Mugabe alidaiwa kusema, “kama tulihitaji watu kwenda Brazil kuimba wimbo wetu wa taifa na kupeperusha bendera, tungewaagiza warembo na vijana watanashati kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe wakatuwakilishe.”

Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ambayo wanamichezo wake hawakufanikiwa kushinda medali ikiwa inawakilishwa na wanamichezo 31. Mchezaji ambaye alionekana kufanya vizuri ni yule aliyekamata nafasi ya nane.

Hata hivyo kuna uwezekano habari hii inaweza kuwa ni ya kutengenezwa (satire) kama nukuu mbalimbali za kuchekesha ambazo amekuwa akidaiwa kuzisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents