Burudani

Mubenga kumrudisha tena Jebby kwenye Bongo Fleva

Bosi wa Bangerz Ent maarufu kwa jina la Mubenga anatarajia kumrudisha tena kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Jebby.

Muimbaji huyo ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wa ‘Swahiba’ aliomshirikisha Afande Sele amesema ameshafanya mazungumzo na bosi huyo na tayari wamekubaliana kwa asilimia hamsini.

“Nilikuwa kimya kwa muda mrefu, nimesoma vizuri game na nimefanya kazi nyingi sana ziko ndani. Sa hizi nikirudi narudi vizuri maana muziki umebadilika sana siku hizi video lazima ziwe kali maana zinafika mbali, hata mtu akiona huko lazima ajue kuwa kweli jamaa amebadilika siyo kama zamani,” amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.

“Mubenga atamrudisha Jebby kwenye muziki nimefanya makubaliano nao kwa asilimia hamsini tushakubaliana,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents