Habari

Mtwara kushika mkia siyo bahati mbaya – Mkuu wa Mkoa

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amesema mkoa huo kutangazwa kushika mkia katika upimaji wa matokeo kidato cha pili siyo bahati mbaya.

Gazeti la mwananchi limeripoti Jumanne hii likisema kuwa licha ya mkuu huyo kutofurahishwa na matokeo hayo alitarajia hali kuwa hivyo kutokana na elimu kutopewa kipaumbele mkoani humo.

“Nimekuja Mtwara nimegundua mambo hayako sawa, nikajaribu kutafuta kiini, ndio nikabaini hakuna mwamko wa elimu, waalimu sio wabunifu, wanashindwa kuangalia mazingira yaliyopo na kufundisha kulingana nayo. Utoro pia umekithiri,” amesema.

Amesema baada ya kugundua kuwa mambo mengi hayaendi sawa katika elimu, ameamua kujiwekea mikakati ya kuanza upya.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents