Habari

Mtu anayesadikiwa kumuua baba mzazi wa rapper STL wa Kenya afungwa jela!

Mwezi January mwaka jana (2012) rapper wa Kenya Stella Mwangi aka STL alimpoteza baba yake mzazi Mr. Jeff Mwangi Kwirikia aliyefariki kwa ajali ya gari huko nchini Norway.

STL n dad

Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Norway mtuhumiwa huyo wa mauaji ya ‘hit and run’ wiki hii (June 4) amehukumiwa kwenda jela siku 120 baada ya kujisalimisha mwenyewe chini ya vyombo vya usalama.

Ikiwa sehemu ya adhabu aliyopewa na mahakama ya Øvre Romerike, mtu huyo mwenye umri wa miaka 40 hatoruhusiwa tena kuendesha gari katika maisha yake, na pia atalazimika kuwalipa fidia wanafamilia kiasi cha NOK 120,000 kila mmoja.

Endapo mtuhumiwa huyo asingejisalimisha mwenyewe polisi na kukili kuwa ndio dereva aliyehusika kumgonga kwa bahati mbaya Mr. Mwangi na kusababisha kifo chake, angehukumiwa miezi mitano jela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents