Burudani

Mtoto wa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow afariki baada ya kuumwa na mbwa

Mtoto wa kiume wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow amefariki baada ya kuumwa na mbwa.

Habibou Barrow alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini kufuatia kisa hicho cha siku ya Jumapili, kilichotokea eneo la Manjai karibu na mji mkuu Banjul.

Mazishi yake tayari yashafanyika.

Bwana Barrow yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa siku ya Alhamisi.

Kwa mjibu wa ripoti hiyo, Barrow ana wake wawili na watoto wengine wanne

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents