Michezo

Mtoto wa Patrick Kluivert, Justin, aichezea Ajax ya wakubwa kwa mara ya kwanza

Mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Uholanzi Patrick Kluivert, Justin Kluivert, ambaye ana umri wa miaka 17 amejitosa kwa mara ya kwanza uwanjani akiwa na klabu ya Ajax na kupata ushindi katika mechi ya ugenini dhidi ya PEC Zwolle siku ya Jumapili.


Justin Kluivert akiingia kuchukua nafasi ya Amin Younes

Justin Kluivert aliingia uwanjani katika dakika ya 39 baada ya Amin Younes kuumia.

Mchezaji Lasse Schone alifunga mkwaju wa penalti nakuifanya Ajax kuwa mbele na Hakim Ziyech akaongeza la pili.

Nicolai Brock-Madsen alikomboa goli moja lakini Ziyech akaongeza jingine na kuwahakikishia Ajax ushindi ambao unaifanya Ajax kusalia na alama tano nyuma ya viongozi Feyenoord.


Justin Kluivert akiwa na Baba yake Patrick Kluivert

Babake, Kluivert Sr, alishinda mataji mawili ya Eredivisie ya uholanzi na pia akashinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya alipokuwa akichezea klabu ya Ajax kwa miaka mitatu kati ya mwaka 1994 na 1997

Alizichezea timu za AC Milan, Barcelona, Newcastle United, Valencia, PSV Eindhoven na Lille na alifunga magoli 40 katika mechi 79 alizochezea timu yake ya taifa.

Patrick Kluivert ambaye kwa hivi sasa ana umri wa miaka 40 ni mkurungezi wa mpira wa soka katika klabu ya PSG. ya Ufaransa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents