Habari

Mtoto wa miaka 15 kutoka Falme za Kiarabu akwea Mlima Kilimanjaro

Mtoto mwenye miaka 15, amekuwa raia wa kwanza kutoka Falme za Kiarabu (UAE) kuwahi kupanda Mlima Kilimanjaro.

3984c031e21df2527fc5209914545863

Ali Saleh Alshunnar, ameupanda mlima huo mrefu zaidi Afrika – mita 5,895. Ni mwanafunzi wa grade 10 Dubai.

January 21, 2008 Keats Boyd kutoka Los Angeles alifanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo akiwa na umri wa miaka 7 tu, na kuwa mtu mwenye umri mdogo kuwahi kufanya hivyo. Mtu mwingine mwenye umri mdogo kuwahi kuupanda mlima huo ni Zain Akrim wa Uingereza. Akiwa na miaka 9 tu, Akrim aliupanda mlima huo tarehe 8, August, 2015.

Naye Angela Vorobeva wa Urusi alikuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuupanda mlima huo. October 29, 2015 kupitia njia ya Machame alifika kileleni akiwa na miaka 86 na siku 267. Naye Richard Byerley alifika kileleni October 2010 akiwa na miaka 84 na siku 71.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents