Habari

Mtazamo: Wasanii wa Bongo Flava ni wengi, kiasi soko la muziki wake limezidiwa?


Muziki wa kizazi kipya umekuwa kwa kiasi kikubwa baada ya jamii kuelewa nini wanafanya wasanii hao. Hii imekuwa changamoto katika muziki huo kutokana na wasanii kuwa wengi kuliko ukubwa wa soko la muziki huo, japo inategemea msanii anaimba muziki wa aina gani.

Ni mtazamo wangu, ingawa itahitaji mawazo ya kila mdau wa muziki kufikiri kwa kina ni nini chanzo cha wasanii kushindwa kuendelea kuwepo kwenye game kwa muda mrefu wakati wanafanya kazi nzuri na zenye ubunifu na huku wengine wakifikiria kwamba ushirikina ndiyo njia ya kumweka mtu juu kimuziki.

Wasanii wengi wamekuwa wakifanya vizuri ila wanaovuma ni wachache, bado sijajua tatizo nini!! . Kuna baadhi ya wasanii wa kizazi kipya ambao tulikuwanao tangu mwanzo ambao kwa sasa hawavumi tena kwenye game. Ingawa bado wanaendelea kutoa nyimbo nzuri, ni jambo la kustaajabisha kuwa zinashindwa kuhit, au tatizo wasanii hao wamechokwa na jamii au jamii imeshindwa kuwaamini tena?

Muziki wa kizazi kipya umekuwa lakini wanaonufaika zaidi ni maharamia wa muziki huo na baadhi ya wadau ambao maisha yao yanategemea kazi za wasanii. Jiulize kwanini wasanii hawatoi tena albam? Hivi sasa baadhi ya wasanii wameamua kuuza albam zao wenyewe. Kama ukweli ni kuwa wasanii wanaonufaika na muziki ni wachache licha ya kuwepo wasanii wengi wenye muziki mzuri, ni kweli soko la muziki halihimili tena wingi wao? Sababu kuna ule msemo kuwa kila nyumba ina msanii! Tafakari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents