BurudaniVideos

Mtazamo wangu juu ya sakata la G-Nako na Nisher kuhusu video ya Arosto

Mapema mwaka huu kupitia mtandao wa Instagram, muongozaji wa video mwenye stunts za kutosha kutoka Arusha namzungumzia Nisher ambaye kwa sasa anataka afahamike kwa jina la Nisher X, alitease kipande cha video ya Arosto na kusema kuwa anasubiri ruhusa ya wenye video ambaye ni rapa G-Nako kutoka kundi la Weusi ambao nao ni wasanii kutoka Arusha.

Nisher 2

Kila aliyeona kipande cha video hiyo alikuwa na mtazamo wake japo kwa wengi walitabiri kuwa itakuwa video kali sana kutokana na aina ya shots alizozifanya Director Nisher X. Ukapita muda sana na ukimya wa kuachiwa kwa video hiyo, nakumbuka mimi binafsi kama mtangazaji wa Kings FM Top 30 nilihitaji kupata studio package ya wimbo wa Arosto. Niliamua kumpigia simu G-Nako na akanipa majibu yuko safarini akifika Arusha nimcheki.

Nikaona itatukuwa muda mrefu zaidi, nikaamua kumpigia simu msanii Quick Rocka ambaye ndiye mmliki wa studio za Switch Records ambako umefanyika wimbo huo chini ya producer Luffa. Majibu ya Abott Charles a.k.a Quick Rocka msanii ambaye nilisoma naye Pandahill Secondary ya jijini Mbeya kidato cha kwanza kisha mimi nikahamia Tosamaganga Secondary. Kwahiyo tumekuwa washkaji kitambo, nilichokipata ni taarifa za awali kabisa kwamba audio haijatoka official sababu kuna matatizo kwenye upande wa video kati ya G-Nako na Nisher X.

Nilitaka kujua ni tatizo gani lakini Quick hakuwa tayari kulisemea hilo na ofcoz alikua sahihi kwasababu sio issue yake. Nikaachana nayo kama ilivyo huku nikisubiri kwa hamu sasa kuona video ya Arosto, lakini jambo la kushtua jana kupitia ukurasa wa Instagram wa Nick wa Pili ambaye ni rapa na msemaji wa kundi la Weusi aliandika video ya Arosto itaachiwa Dodoma na imeongozwa na Director Hanscana “What a suprise”.

Nikaamua kufuatilia zaidi kujua kunani, nikakutana na post za video za kujieleza saba kutoka kwa director Nisher kwenye IG yake akilalamika sana kuhusiana na kitu alichokifanya G-Nako kuachana na video aliyoongoza yeye na kwenda kuifanya nyingine kwa Hanscana.

Katika maelezo ya Nisher X amedai kuwa Video ya Arosto imeshutiwa kwa gharama zake yeye ambazo zinafikia milioni 3 na laki 9. Ukiacha alizotoa G-Nako mwenye kuwalipa washkaji zake na chakula tu. Nisher alitoa conditions ambazo zilikuwa zinaonesha kutoridhishwa na kitendo alichofanya G-Nako ambaye aliyedai kuwa video aliyoshoot Nisher haijatisha kabisa.

Nisher aliomba kurudia baadhi ya sehemu zenye matatizo ili kumridhisha mteja wake lakini bado haikumpendeza G-Nako, na huenda ndio sababu ya kwenda kwa Hanscana kuirudia video hiyo. Japo inaonekana hakuna makubaliano juu ya hilo kati ya Nisher na Weusi. Nisher aliamua kutoa msimamo wake kwamba endapo G-Nako ataiachia video iliyoongozwa Hanscana basi naye ataiachia ya kwake ili tu watu wapime wenyewe.

Jana usiku video ya Arosto iliyoongozwa na Hanscana iliachiwa rasmi, haukupita muda mrefu Nisher naye akaachia version yake. Jambo hilo limeweka sintofahamu kubwa kwa mashabiki na kuzidi kuongeza beef kati ya Nisher na Hanscana pia kuongeza idadi ya watu ambao Nisher ametofautiana nao kikazi (Kundi la Weusi).

Tukirudi sasa kwenye sababu za msingi za tofauti za video hizi mbili, kwa mtazamo wangu kama mfuatiliaji wa masuala ya muziki, nimeziangalia video zote mbili kwa zaidi ya mara 10 mpaka sasa nikitafuta makosa na usahihi wake.

Nilichokibaini binafsi tukianzia kwenye suala la rangi. Ukiangalia video ya Arosto iliyoanza kutoka kwa Hanscana ina rangi ambayo ina uhalisia sana watu vitu na watu jambo ambalo huenda ndio sababu kubwa sana ya Weusi kuhamia kwake, ila ukija kwenye suala la shots bado ni za kawaida sana, haina tofauti na video za nyimbo za injili. Pia mixing ya audio haisound vizuri.

Wakati kwa video ya Nisher sasa naliona tatizo la rangi zisizo na uhalisia (natural colour) ya vitu haiko sahihi, kitu ambacho Nisher amekuWa akisemwa sana kuwa nacho. Watu na vitu vinakosa uhalisia wa rangi zao sababu ya kuunguzwa sana kwa rangi, ila tu suala la shots zile nampa shkamoo za kutosha Nisher X hapo hakuna wa kupinga jamaa anajua sana kucheza na Camera. Pia suala la mixing ya audio iko good as u know jamaa ni producer pia wa music.

Kwa ujumla hapa suala hili limekosa busara tu ya kukaa chini kwa hawa jamaa na wakamaliza tatizo ila kwa kilichofanyika hapa kuna kugawana mashabiki sasa na huenda ikawa tatizo kwenye kufanya vizuri video hii kwenye TV za kimataifa na inaeza isiende kabisa. Lakini pia tayari Nisher anakuwa amepoteza wateja, na Weusi wamepoteza muongozaji mkali sana wakati Hanscana amepata wateja wapya na kuendelea kuongeza fanbase yake. Ushauri: Jamaa wakae chini waondoe tofauti zao ili kuendelea kusukuma music industry ya Tanzania isogee mbele.

NA KING DAVID, Programs Director KINGS RADIO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents