Burudani

Mtaalamu wa masoko na ‘branding’ atua bongo kusaka wasanii (Video)

Mtaalamu wa makosoko na branding wa Young Media Foundation kutoka nchini Kenya, Beatrice Ndung’u ametua jijini Dar es salaam wiki hii kwa ajili ya kusaini wasanii ambao atawapiga msasa kuhusu kujibrand pamoja na jinsi ya kutafuta masoko mapya ya kazi zao.
Beatrice
Beatrice Ndung’u

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Beatrice Ndung’u amesema amefanya research na kugundua Tanzania kuna wasanii wengi ambao wanahitaji branding.

“Nimefanya utafiti na nimeona Tanzania kuna vipaji vingi sana, kuna waigizaji, wasanii wa muziki, na kwa kazi yangu ya Public Relation ambayo imenileta, nikuwabrand pamoja na kuwatafutia masoko zaidi,” alisema Beatrice.

Aliongeza, “Nataka kuwasaini kwa sababu kuna wasanii wengi sana hapa wanavipaji lakini wanajulikana hapa hapa Tanzania, ukienda Kenya ukauliza watu wanasema hawamjui lakini Tanzania amehit, kwa hiyo kazi yangu ni kuhakikisha hawa wasanii wanajulikana nje ya nchi zao, Kenya , Uganda na Rwanda. So kazi yangu ni kuhakikisha huyo msanii amejulikana kila sehemu kwa kupitia interview pamoja na branding,”

Beatrice amesema tayari ameshafanya mazungumzo na baadhi ya wasanii akiwemo, Abdul Kiba na Belle 9.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents