Burudani

Mtaa aliojenga Chege kuitwa ‘Chege Street’!


Chege Chigunda ‘Mtoto wa Mama Said’ anaweza kuwa msanii wa Bongo Fleva aliyepewa heshima zaidi pengine kuliko wote Tanzania.

Hii ni kwasababu majirani katika mtaa aliojenga nyumba yake wamekubaliana kuuita mtaa huo kwa jina lake, ‘Chege Street’.

Mtaa huo upo maeneo ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.

Akiongea na XXL ya Clouds FM jana, Chege amesema majirani zake ambao wengi ni ‘mambo safi’ wamependekeza jina hilo ili kuufanya mtaa huo uwe maarufu mapema na kuvutia biashara zao!

Cha kushangaza zaidi ni kuwa nyumba hiyo ameijenga kwa mwezi mmoja tu na sasa inamsubiri yeye kuhama alikopanga na kuingia kwenye nyumba yake mpya ambayo anasema akiwa ndani huburudishwa na sauti za wafungwa wa gereza la Segerea lililo jirani kabisa.

Kabla hatujasau, Chege amesema anasikia Lady Jaydee naye kaporomosha mjengo mwingine mitaa hiyo hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents