Burudani

Msimu wa pili wa ‘In My Shoes’ ya Wema Sepetu kuanza wiki Ijayo, Diamond kuonekana ndani

Kama unamfuata Wema Sepetu kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii sina shaka uliona picha akiwa nje ya nchi hivi karibuni na timu yake, hayo yote yalikuwa ni maandalizi ya msimu wa pili wa reality show yake ya Tv ‘In My Shoes’.

wd

Wema amesema msimu mpya utakuwa na maboresho mengi na surprises nyingi.

“Sasa hivi tumekuja kwa kasi flani hivi, wanasema mwanzo ni mgumu na season ya kwanza kiukweli ilikuwa ngumu lakini kuna mengi ambayo tumejifunza, kuna mabadiliko mengi, kwahiyo ni kama ime advance”.
Wema ameiambia Power Jams ya EA Radio.

wema na chibu 2

Kuhusu mpenzi wake Diamond kuonekana kwenye msimu mpya wa ‘In My Shoes’ wema amesema:

“Wote si tutamuona, yaani kwenye episode ya kwanza tu anaonekana, so tutamuona, there will be a lot of Nasib kwasababu most of the times ndio niko nae he is my baby kwahiyo tutaona vitu vingi vingi”.

Kipindi hicho ambacho huonesha maisha halisi ya Wema ambaye ni Miss Tanzania wa mwaka 2006, hivi sasa kitakuwa kikiruka siku za Ijumaa kuanzia saa tatu na nusu usiku kupitia EATV.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents