Msimu mpya wa Big Brother Africa 2014 unaotarajiwa kuanza Septemba 7 utaitwa ‘Hot Shots’
Msimu wa tisa wa reality show maarufu ya Big Brother Africa 2014 unaotarajiwa kuanza Jumapili Septemba 7, utafahamika kama ‘Hot Shots’.
Wawakilishi wa jumla ya nchi 14 watakuwa wakishindania zawadi ya dola laki 3 ambazo zitakabidhiwa kwa mshiriki mmoja atakayedumu kwa siku 91 za shindano na kuibuka mshindi.
IK
Mnigeria IK ndiye atakuwa host wa Big Brother Africa 2014 ‘Hot Shots’ kwa mara ya 5 mfululizo.
Mkurugenzi wa M-Net Africa kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu amesema watazamaji watarajie surprise nyingi katika msimu huu.
“We work hard to make each season of Big Brother Africa bigger than the last — and we have really upped the ante this year,” Alisema.
Big Brother Africa 2014 itakuwa ikionekana kupitia DSTV Channel 197 na 198.
Source: Bigbrotherafrica2014