Habari

Mshauri wa Donald Trump, Michael Flynn ajiuzulu

By  | 

Michael Flynn ambaye ni mshauri mkuu wa ikulu ya Marekani kuhusu usalama wa taifa, amejiuzulu katika nafasi hiyo usiku wa Jumatatu hii kuhusiana na uhusiano wake na maafisa wa Urusi.

Inadaiwa kuwa mwezi uliopita kabla Donald Trump hajakabidhiwa madaraka ya Urais, Flynn alijadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi akiwa na balozi wa Urusi huku akidaiwa kutoa taarifa zisizo za ukweli juu ya mazungumzo hayo kwa maafisa wa utawla wa Trump.

Soma barua hiyo hapa chini iliyotolewa na CNN ambayo imeandikwa na Flynn ya kujiuzulu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments