Burudani

Msechu: Ukubwa wa Nyota unanipa wakati mgumu kuja na ngoma ya kuizidi

Peter Msechu amesema kwa jinsi wimbo wake Nyota ulivyofanya vizuri, anashindwa kupata wimbo mwingune utakaoweza kufanya vizuri zaidi yake.

11313721_433097830210023_61469450_n

Msechu ameiambia Bongo5 jana kuwa licha ya kuwa tayari ana nyimbo nyingi amerekodi, anaona hazina nguvu kama Nyota iliyotangulia.

“Sasa nipo kwenye maandalizi ya video mpya pia nina kazi nyingi ambazo zipo tayari lakini napata wakati mgumu kupata wimbo ambao utau-replace Nyota,” amesema. “Tayari ni nyimbo nyingi nimerekodi lakini naona bado.”

“Kazi zipo nyingi sana, ila ukipita uchaguzi ndio nitajua sasa naachia ngoma gani katika nilizonazo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents