Burudani

Msechu aeleza kwanini hawezi kuwa na wivu kwa mchumba wake

Peter Msechu amesema anampenda na kumwamini mke wake.

Peter Msechu na Mpenzi wake

Akizungumza na E-Newz ya EATV, Msechu alisema mchumba wake aliyezaa naye mtoto mmoja wamefahamiana tangu mwaka 2002.

“Namwachaje mwanamke nimemganda kama luba, hata nimkute na wanaume 4000 namwambia ‘mama kaoge tuendelee na maisha,” alisema alisema Mchechu.

“Maisha ni mazuri sana, mama wa mtoto wangu nimekutana naye mwaka 2002, hesabu huu ni mwaka wa ngapi nipo na huyu mama? Na huyo mama ndio aliyenipigia simu akaniambia ‘mpenzi wangu BSS inakuja Kigoma, ukiweza kumaliza form six njoo ujaribishe kwa sababu unaimba vizuri sana kanisani.’

Kwahiyo yeye alivyoniambia hivyo mtihani wa mwisho wa Economics 2 nilifanya swali moja tu lile la compulsory nikaachana nao nikawahi basi la mwisho la Tanga. Kwahiyo yeye kauli yake ndio nikawahi Kigoma nikatusua ndio nikaanza muziki mpaka leo.”
.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents