Burudani

Msanii wa Tanzania aishiye Dubai, Jeff Maximum aja Dar kushoot video ya ‘Mama Africa’

Msanii wa Tanzania aliyehamishia makazi yake Dubai, Jeff Maximum ameamua kurejea nyumbani kushoot video ya wimbo wake mpya, Mama Africa.

CMNj-YVUYAA7r1C

Alianza muziki akiwa Tanzania miaka 18 iliyopita kabla ya kuhamia jijini Los Angeles na hatimaye Dubai. Jeff anayefanya muziki wa R&B, hufanyia kazi zake Marekani, Dubai na Singapore.

Hanscana ndiye anayeiongoza video ya wimbo huo. Amesema ameamua kuja kufanya video yake Tanzania kwakuwa ni nchi inayosifika kwa amani duniani kote na ina mandhari ya kuvutia.

“Kila ninapotembelea nchi zote nikiwa Tanzania najihisi nipo nyumbani, sijawahi kuishi hapa kwa kipindi kirefu lakini najisikia amani zaidi nikiwa hapa kuliko sehemu nyingine yoyote. Nimeishi Marekani, Singapore, Dubai lakini kote naona nipo ugenini,” amesema.

Kabla ya wimbo huo, Jeff amewahi kutamba na nyimbo ‘Stay With Me’ na ‘Forever.’

Pamoja na kuja kufanya video, Jeff anatoa fursa ya kuwasaidia wasanii wenye vipaji na kwaMba wamtumie kazi zao kwa email yake [email protected] au kumfuata kwenye mitandao ya kijamii kwa jina la @jeffmaximum.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents