Burudani

Msanii wa Nigeria Runtown awataja wasanii wawili wa Tanzania anaowakubali zaidi

Mwimbaji kutoka Nigeria, Runtown ametua jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo (Oct.9) tayari kulipamba jukwaa la fainali ya shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search (BSS) itakayofanyika Ijumaa (Oct.9).

runtown (1)

Kama ambavyo wasanii wetu wanafuatilia kwa karibu muziki wa Nigeria, Runtown pia anafatilia muziki wa Bongo. Katika mahojiano mafupi na Fahamu Tv, Runtown amewataja wasanii wawili wa Bongo anaowakubali zaidi. Alianza kumtaja hit maker wa ‘No Body But Me’ Vanessa Mdee kwa upande wa wasanii wa kike, pia akamtaja Diamond na kusema kuwa ndiye msanii namba moja anayemkubali zaidi kwa wasanii wa kiume wa Tanzania.

Runtown pia amethibitisha kuwa amefanya collabo na Chege, na kuongeza kuwa kuna collabo nyingine atakazofanya na Diamond na Vanessa.

Hizi ni baadhi ya nyimbo/video za Runtown zilizofanya vizuri. Gallardo aliyomshirikisha Davido, ‘The Latest’ pamoja na ‘The Banger’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents