Burudani

Msanii wa Nigeria Burna Boy aponda mfumo wa muziki wa Nigeria, adai umejaa siasa

Muimbaji wa Dancehall kutoka Nigeria, Burna Boy ameponda mfumo wa muziki wa Nigeria na kudai kuwa umejaa siasa ndio sababu hapati tuzo nyingi anazostahili.

Burna-Boy

Akizungumza na jarida la Fader, Burna amesema kutokana na hayo anajiona kama yeye si sehemu ya muziki wa Nigeria kwasababu kuna baadhi ya watu walioutawala muziki huo wasiompenda.

“Kusema kweli ni siasa tupu, sijioni kama ni sehemu ya kiwanda cha muziki, angalia tuzo, sipati tuzo kwasababu wanaoutawala hawanipendi, mimi sio kama wengine, siwezi kufanya kama wafanyavyo wengine, hawapendi hicho”.

Muimbaji huyo wa ‘Check and Balance’ ameongeza kuwa licha ya kuwa hana wafuasi wengi Instagram na Twitter lakini anaamini anafanya vitu vizuri na vikubwa kuwazidi wasanii wengine wenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents