Burudani
Msanii huyu wa Kenya kutumbuiza pamoja na KCEE na Bracket wa Nigeria nchini Switzerland
Msanii wa Kenya, Esther Akoth maarufu kama Akothee ataungana na wasanii wa Nigeria, KCEE na kundi la Bracket kutumbuiza jijini Zurich, Switzerland mwezi ujao.
Hivi karibuni Akothee alimake headlines baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kusherehekea Valentine’s Day.
Muimbaji na mfanyabiashara huyo wa Mombasa alikodi gari ndefu ya Limousine kwa masaa matano ambapo kila saa alilipa shilingi 40,000 za Kenya.