BurudaniVideos

Msafiri adai walishoot video ya Chafu Pozi ya Bill Nas kwenye maeneo hatari zaidi SA

Muongozaji wa video za muziki wa kampuni ya Kwetu Studios, Msafiri, ameitaja video ya Bill Nas ya wimbo wake Chafu Pozi kuwa ndiyo ilimuwia vigumu zaidi kuikamilisha.

Akizungumza kwenye kipindi cha Amka na Choice cha Choice FM kinachoendeshwa na Divine Kweka, wiki iliyopita, Msafiri alisema maeneo waliyoshoot video hiyo ni ya hatari zaidi Afrika Kusini.

“Tumeshoot Johannesburg sehemu inaitwa Soweto, ndio hiyo sehemu inaitwa Chafu Pozi. Ni video ambayo ilitupa wakati mgumu sana kwasababu mara nyingi video tunazoshoot South Africa tunaenda kwenye hotels au apartment, tunakuwa na uhuru wa kufanya tunachotaka. Kwasababu nchi kama South Africa mtu anaweza akaja na bunduki akachukua kamera yako, akachukua simu, akachukua hela yako akaondoka,” alisema muongozaji huyo.

“Kwahiyo ni video ambayo tumefanya katika mazingira hatarishi, ukinirudisha leo lazima nikuchaji extra charges kwasababu ya mazingira yenyewe,” aliongeza.

Msafiri ni moja ya waongozaji wa video za muziki nchini wanaokubalika zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents